Latest News

Utapiamlo umeendelea kuathiri jamii ya ki-Tanzania

Tunaelewa wazi kuwa pamoja na maendeleo ambayo nchi yetu imekuwa ikiyapata katika maeneo mbalimbali, bado utapiamlo umeendelea kuathiri jamii ya ki-Tanzania hususan kiafya, kielimu na kiuchumi na hivyo kusababisha kasi ya kupungua kwa umaskini nchini kuwa si ya kuridhisha. Lishe duni si tu inaathiri maendeleo ya mtoto lakini pia inaathiri ukuaji wake kimwili na kiakili na hatimaye kuathiri mchango wake katika maendeleo ya taifa katika kipindi chote cha uhai wake.Takwimu za hivi karibuni zimebaini kupungua kwa viwango vya kitaifa vya utapiamlo hasa kwa watoto kwa viashiria vya Udumavu, na Uzito pungufu ukilinganisha hali ilivyokuwa mwaka 2010. Udumavu umepungua kutoka asilimia 42.8 hadi 34.4 na Uzito Pungufu kutoka asilimia 16 hadi 14. Lakini kiwango cha ukondefu kimeongezeka kutoka asilimia 3.8 hadi 5 Kwa mkoa wetu wa Tabora, Udumavu umepungua kutoka asilimia 33 hadi 27, na Uzito Pungufu kutoka asilimia 11 hadi 10. Lakini kiwango cha ukondefu kimebaki palepale asilimia 4 Pamoja na kupungua kwa viwango hivi bado inakadiriwa kuwa kuna zaidi ya watoto milioni 2.7 ambao wamedumaa nchini ambao wengi wao wapo katika mikoa 10, mkoa wetu wa Tabora ukiwemo. Vilevile, imebainika kuwa kaya nyingi hazitumii chumvi yenye madini joto tika ya mikoa 10 inyoonesha kiwango kidogo zaidi cha matumizi mkoa wetu ni mojawapo (Tabora (19.5%), Ikumbukwe kuwa matumizi duni ya chumvi yenye madini joto huongeza uwezekano mkubwa wa watoto kuvia kiakili.Lakini pia imebainika jamii zetu hazitumii sabuni wakati wa kunawa mikono hasa baada ya kutoka chooni na kabla ya kula chakula,Mikoa 6 iliyopata chini ya asilimia moja (1%) kwenye matumizi ya sabuni mkoa wetu ni mojawapo ukiwa na asilimia sifuri (Tabora 0.0%). Hali ya lishe ya wanawake nayo bado ni mbaya.kati ya wanawake kumi mmoja kati yao ana utapiamlo, sote tunapaswa kufahamu lishe duni kwa wanawake wajawazito inawaweka katika mazingira yanayoweza kusababisha kujifungua watoto njiti au kuharibu mimba. Asilimia 55 ya wanawake wa Tabora wana upungufu wa damu unaochangia kupoteza maisha wakati au baada ya kujifungua. Vifo vya wanawake wajawazito vitapungua sana endapo watakuwa na hali nzuri ya lishe katika kipindi chote cha ujauzito.